Home KITAIFA JUMLA YA CHUPA 495,600 ZA DAMU ZAKUSANYWA KATIKA MIKOA 15

JUMLA YA CHUPA 495,600 ZA DAMU ZAKUSANYWA KATIKA MIKOA 15

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu ameelekeza vituo vya afya vya Serikali vinavyotoa huduma ya upasuaji Kununua majokofu ya kuhifadhia mazao ya damu lengo ni kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.

Ummy ameseyasema hayo Juni 14,2023 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya mchangia damu duniani na uzinduzi wa huduma ya damu salama kituo cha kanda ya kati Dodoma.

Amesema kuwa katika kuhakikisha wakinana mama wajawazito wanapatiwa damu kila inapohitajika kila kituo cha afya kinachotoa huduma ya upasuaji kinunue majokofu kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya damu.

Hata hivyo mazao ya damu kuwa ni chembe hai nyekundu,, chembe Sahani ambazo huwasaidia wagonjwa wenye saratani na plasma kwa ajili ya wajawazito ambapo mpaka sasa Zaidi ya chupa 23,000 zimetumika kwa ajili ya wajawazito.

‘’ Kila vifo 43 kati ya wajawazito 100 vinatokana na kuvuja damu nyingi wakati wa kujifungua lakini kama damu ikipatikana kwa wakati kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza vifo hivyo.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kila watu 100 angalau kuwepo na chupa moja ya damu, ambapo kwa Tanzania kwa mwaka chupa za damu zinazohitajika ni 590,000.

Waziri huyo alisema kuwa kuanzia sasa wataanzisha tuzo kwenye mikoa na halmashauri zitakazikusanya sana damu ambapo mikoa mitatu na halmashauri tatu zitapata tuzo hizo lengo ni kuwatia moyo na kuhamasisha shughuli za uchangiaji damu.

Amesema kwa mwaka 2022/2023 jumla ya chupa 495,600 za damu zilikusanywa, mikoa 15 ilifanikiwa kukusanya damu na kukidhi mahitaji kutokana na uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo aliagiza kuanzia sasa Wizara ya afya inabeba gharama za mafuriko ya kukusanyia damu bure.Pia aliagiza Idara ya huduma za uzazi mama na mtoro kwa kushirikiana na damu salama kujengewa uwezo juu ya matumizi sahihi ya mazao ya damu.

“Damu inapokusanywa muda wake wa kukaa ni siku 45 tu, lakini mazao yad amu hutumika kwa mwaka mzima, ndiyo maana matumizi ya mazao yad amu yamekuwa yakisisitizwa ili kuongeza muda wad amu kutumika,” amesema.

Pia ameziagiza halmashauri zote 184 nchini kutenga bajeti ili kurahisisha ukusanyaji wa damu ambapo sasa Wizara ya afya imebeba gharama ya mifuko ya kukusanyia damu na hutolewa bure.

Maadhimisho hayo yalibeba kauli mbiu, changia damu, changia mazao ya damu (plasma), changia mara kwa mara, pia yaliambatana na utoaji wavyeti, zawadi kwa wachangia damu na taasisi zilizofanya vizuri Zaidi, aidha uzinduzi wa kadi za kielektroniki za wachangia wa mara kwa mara .

Previous articleSIMBACHAWENE AKIRI MAPUNGUFU SHERIA LIKIZO YA UZAZI
Next articleWAFAMASIA MLOGANZILA WATOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA KWA WANAFUNZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here