MAKAMU wa Rais DK.Philp Mpango ameliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT )kuwekeza nguvu kwa Vijana katika kuwafundisha matumizi ya Teknolojia katika suala Zima la uzalishaji wa Chakula ili Nchi iweze kuwa Ghala la Chakula Ukanda wa Afrika huku akisistiza suala la utunzaji wa vyanzo vya Maji na uhifadhi wa Mazingira.
Dk.Mpango ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Maadhimisho ya Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Mwaka 1963 yanayoenda sambamba na maonyesho ya bidhaa mbalimbali.
AKizungumzia kuhusiana na Maadhimisho hayo,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Innocent Bashungwa amesema kuwa kama Jeshi watatekeleza maagizo ya Makamu wa Rais kwakuyafanyia kazi.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje,Ulinzi na Usalama, Victor Kawawa amesema kama Kamati wanaridhishwa na kazi za Jeshi hilo huku wakiishauri Serikali kuongeza muda wa mafunzo ya JKT kwa Vijana wanaochaguliwa kuingia Kidato cha sita badala ya miezi mitatu iwe miezi sita na mafunzo yawe kwa Vijana wote.