Home KITAIFA JKT KUTUMIA ZAIDI YA BILIONI 9 KUENDELEZA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAKAMBI...

JKT KUTUMIA ZAIDI YA BILIONI 9 KUENDELEZA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAKAMBI YA VIJANA

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 linaratajia kutumia jumla ya Sh bilioni9.96 kwaajili ya kuendeleza na kuboresha miundombinu ya Makambi ya Vijana pamoja na kuongeza Makambi mengine mapya ili Vijana wengi waweze kujiunga na mafunzo ya mujibu wa Sheria kwakuwafanya kuwa wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu yake na mwelekeo wa Bajeti kwa Mwaka 2023/2024 julai 27,2023 jijini Dodoma Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajab Mabele amesema ongezeko la vijana wanaojiunga na Jeshi kwa mujibu wa sheria kutoka vijana 26,000 mwaka 2022/2023 hadi 52,119 mwaka 2023/2024 ikiwa ni ongezeko la asilimia 54.

Ameongeza kuwa Ongezeko hilo limepatikana kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuliwezesha jeshi hilo.

Pamoja na hayo amesema Jeshi hilo limejipanga katika suala zima la uzalishaji ikiwemo kilimo na ufugaji ili Tanzania kuweza kuwa Ghala la Chakula.

Amesema mipango waliyonayo ya kuwaunganisha vijana wa Jeshi hilo na mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT),unaotekelezwa na Wizara ya Kilimo, “azma ya serikali ni kuchukua vijana wote wanaomaliza kidato cha sita ili wahudhurie mafunzo ya lazima,”.

JKT ilianzishwa rasmi mwaka 1963 ikiwa na majukumu mbalimbali ya msingi ikiwemo malezi ya vijana ,ulinzi wa Taifa na uzalishaji mali.

Previous articleTANI 700 ZA SALFA ZIMEPOKELEWA PWANI
Next articleTASAC KUNUNUA BOTI TATU ZA UOKOZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here