Na Theophilida Felician Kagera.
Mkaguzi msaidizi na kaimu Mkuu wa Jeshi la zima Moto na uokoaji wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera Abdara Muhidini Ngaugia amesema kuwa baada ya kutokea tukio la Moto uliozuka na kuunguza duka moja na bidhaa zilizokuwemo kuteketea katika soko kuu la Manispaa ya Bukoba tayari Jeshi hilo limeanza kufanya uchunguzi kwa kina ili kuweza kubaini nini chanzo kilichosabaisha mkasa wa moto huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo baada ya kufika eneo la tukio kuanza zoezi la uchunguzi amesema kuwa mnamo tarehe 21 May mwaka huu usiku wa kumkia leo majira ya saa tatu na dakika 3: 43 jeshi hilo lilipokea taarifa za kuwepo kwa tukio la kuwaka moto maduka ya soko kuu hivyo liliwahi kufika sokoni hapo hatimaye kuanza kazi ya kuuzima hivyo kufikia mida ya saa sita 6 usiku hali ilikuwa tulivu na moto ulikuwa umedhibitiwa tayari.
“Sisi baada yakufika hapa tulikuta duka hili moja la mfanya biashara Ibrahimu Karwani likiwaka Moto kweli kweli kwakushirikiana na wenzetu wa Polis na TANESCO tuliudhibiti ipasavyo na haukuendelea kusambaa katika maduka mengine japo maduka ( 2) jirani na duka la Ibrahimu yaliathiriwa ila kwakiwango kidogo” amefafanua Kaimu Mkuu Abdara Muhidini.
Amevitaja baadhi vitu vilivyokuwemo ndani ya duka hilo ni pamoja na magodoro, nguo na mabegi na vinginevyo.
Ameongeza kuwa thamani ya mali zilizoteketea ndani ya duka la Ibrahimu haijafahamika bado hivyo baada ya uchunguzi kila kitu kitafahamika kwa undani.
Amesema baada ya uchunguzi na kupatika taarifa sahii itatolewa kwa umma.
Leonidas Leopodi mmoja wawenye maduka jirani na Ibrahimu Karwani aliyekutwa na takio la kuunguliwa duka lake ameeleza kwamba wakati tukio linatokea alikuwa tayari kafunga duka na kuondoka, akiwa nyumbani alipokea taarifa za kuungua maduka yao baada yakufika alikuta duka lake likiwa limebomolewa ili kufanya kazi ya uokozi wa bidhaa zake.
“Na mshukuru Mungu Mimi hapa nimeathiliwa na moshi wa Moto uliokuwa ikitokea kwenye duka hili la mwenzetu kiukweli kwetu hatujapata madhara makubwa kama Ibrahimu tunashukuru sana Jeshi la zima Moto na uokoaji limetusaidia kuudhibiti moto huu bidhaa zetu zimabekia salama vinginevyo maduka mengi hapa yangelitekete mno tofauti na hali tunayoishuhudia hivi sasa” amehadithia Leonidasi Leopodi.
Pia meliomba Jeshi hilo kuendelea na juhudi kama hizo walizozionyesha katika tukio hilo pale yanapokuwa yametokea matukio ya namna hiyo katika jamii.