Home KITAIFA JESHI LA UHAMIAJI MWANZA WAPATA TUZO YA UTOAJI HUDUMA BORA KATIKA MAONESHO...

JESHI LA UHAMIAJI MWANZA WAPATA TUZO YA UTOAJI HUDUMA BORA KATIKA MAONESHO YA AFRIKA MASHARIKI

Katika maonesho ya 18 ya Afrika Mashariki yanayoendelea katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Jeshi la uhamiaji Mkoa wa Mwanza limepata tuzo ya mtoa huduma bora katika kundi la serikali kuu ambapo imepata kombe pamoja na cheti kutoka kwenye mamlaka ya Chemba ya wafanyabiashara mkoa wa Mwanza kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Jeshi hilo.

Huduma za uhamiaji zilizopewa kipaumbele katika maonesho hayo ni pamoja na utoaji wa huduma za elimu kuhusu pasport,utoaji wa vibali vya ukaazi na huduma za uhamiaji kwa wageni.

Jeshi la Uhamiaji mkoani humo limekuwa likitoa huduma bora na za haraka kwa wateja wake na hii ni fursa nzuri ya kuwafikia wananchi na kujibu maswali yao kuhusu taratibu za uhamiaji.

Kupitia banda la maonesho hayo Jeshi hilo limeweka timu ya wataalamu wenye uzoefu ambao wanajibu maswali na kutoa ushauri kwa wageni wanaohitaji huduma mbalimbali.

Jeshi hilo linashiriki katika Maonesho ya 18 ya Biashara ya Africa Mashariki yaliyoanza tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu na yanatarajiwa kutamatishwa Septemba 3 mwaka huu huku yakiwa na kauli mbiu isemayo, Mazingira Bora ya Biashara ni kivutio cha kukuza uwekezaji wa Biashara, Viwanda na Kilimo Africa Mashariki.

Ambapo maonesho hayo yanafanyika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza na yameandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara mkoani humo, aidha maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 28 Septemba hivi karibuni na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe ( Mb ) Maonesho hayo yamejumuhisha washiriki mbalimbali kutoka nchi za Africa Mashariki.

Previous articleWENYE MASHAKA AU WASIWASI NA DIRA (MITA) ZA MAJI WAENDE WAKALA WA VIPIMO (WMA) KWA UHAKIKI
Next articleSERIKALI YAWAVAA VIKALI WANASIASA, KISA KUINGIZA SIASA KATIKA KILIMO_ MAGAZETINI LEO JUMATATU SEPTEMBA 04/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here