Home KITAIFA JESHI LA POLISI LIMETOA MAFUNZO YA KUBAINI, KUZUIA NA KUKABILIANA NA UHALIFU.

JESHI LA POLISI LIMETOA MAFUNZO YA KUBAINI, KUZUIA NA KUKABILIANA NA UHALIFU.

 

Jeshi la Polisi Tanzania limetoa mafunzo ya pamoja kati ya jeshi la hilo, watendaji wa kata viongozi wa dini , madiwani ,wenyeviti wa mtaa yenye lengo la kuwajengea uwezo jinsi ya kushirikiana katika kubaini ,kuzuia na kukabiliana na uharifu, na jumla ya askari polisi 280 wameshiriki mafunzo hayo.

Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii Faustine Shilogile amesema jeshi la polisi Tanzania litaendelea kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwa vizuri kama ilivyo hivi sasa.

“Nikupongeze Mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makala pamoja kamati yako ya usalama kwa ujumla mkoa wako huko shwali makao makuu tunapokea taarifa ya mikoa yote nah ii yote nikutokana na juhudi yako ya kusimamia mambo ya usalama katika mkoa mzima, Faustine Shilogile” Kamishna wa kamisheni ya polisi jamii.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makala,amelipongeza Jeshi la polisi kwa kuwafikia wananchi katika maeneo yao huku akipongeza utaratibu wa kuweka polisi jamii katika kata kutaimarisha masuala ya usalama katika maeneo hayo.

“ Lakini niwakumbushe pia jukumu la kupunguza uhalifu ni jukumu la jamii nzima ndio maana wenzetu wa jeshi la polisi mkaja na dhana ya polisi jamii ambayo ni muunganiko chanya baina ya jeshi hilo na wananchi katika masuala ya mazima ya kupambana na uhalifu, Amos Makala “Mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Previous articleJESHI LA POLISI LATOA TAMKO GARI LA CHADEMA KUCHOMWA MOTO GEITA
Next article“WAUZAJI WA VIUATILIFU KUWENI NA MAJAWABU YA KUJITOSHELEZA KWA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI” SILINDE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here