Home KITAIFA JESHI LA POLISI LAWAHIMIZA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI SIMIYU

JESHI LA POLISI LAWAHIMIZA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA VITENDO VYA UKATILI SIMIYU

Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi -Simiyu

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu limewahimiza wanachi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili mkoani humo vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu.

Kauli hiyo imetolewa Agosti 27,2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe wakati wa sherehe za mavuno katika Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Ushirika wa Tumaini Bariadi alipopata nafasi ya kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia.

ACP Swebe ameongeza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia nyumba za ibada kukemea vitendo viovu pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia unafanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu.

Amewaomba wazazi kuongeza ulinzi kwa watoto ambapo amebainisha kuwa kundi hilo kwa sasa ukiangalia takwimu ndio waathirika wa kubwa dhidi ya vitendo vya ukatili huku akiwaomba kutoa taarifa hizo kwa vyombo husika.

Pia kamanda swebe amesema vitendo vya ukatili vinarudisha nyuma maendeleo kwa makundi yote yanayofanyiwa ukatili katika jamii.

Sambamba na hilo amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuiombea nchi na Mkoa wa Simiyu ili kuendelea kuwa shwari

Previous articleTAKUKURU MBEYA YAWABURUZA 14 MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI
Next articleWANANCHI WAPEWA RAI KUSHIRIKI WIKI YA KITAIFA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here