Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa, amelielekeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) hadi kufikia Oktoba mwaka huu, kuendelea na mradi wa ujenzi wa nyumba wa 711 (Seven Eleven ) uliopo Kawe jijini Dar es Salaam ili kupunguza ongezeko la fedha za ujenzi huo uliokwama kwa muda mrefu na kutoa unafuu kwa watanzania wenye mahitaji ya nyumba.
Hayo ameyaeleza jana katika ziara yake ya kwanza ya kukagua miradi ya shirika hilo chini ya Wizara yake, ikiwemo mradi wa Samia Housing Scheme unaohusisha ujenzi wa nyumba 560 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 48 na Mradi wa Morocco Square uliogharimu bilioni 137.5 ambao hadi sasa umefikia asilimia 98, ikiwa na lengo la kujionea hali ya maendeleo ya ujenzi katika miradi hiyo.
Pia Waziri Silaa amewataka NHC kuongeza wigo wa Mradi wa Samia Scheme na kuhakikisha unafanyika katika mikoa mingine, hususani kwenye majiji makubwa yenye mahitaji ya nyumba ya kiwemo Dodoma, Mwanza na Arusha.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah amesema shirika hilo lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kupitia fedha zinazopatikana kwenye ajira zinazozalishwa na uzlipaji wa kodi za Serikali. na kuwa hadi kufikia Disemba 1, 2023 Mradi wa Morocco utakuwa umeanza kazi kwa sehemu kubwa. huku wakiahidi kutekeleza maelekezo ya waziri ya kukamilisha michakato ili kuendeleza mradi wa 711 uliotakiwa kukamilisha 2017 kabla ya kukwama, kwa gharama ya awali ya bilioni 107″_ Alisema.