Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Selemani Jafo ameyataka mabonde yote nchini kuendelea kuhamasisha zoezi la upandaji wa miti pamoja na kusafisha kingo za vyanzo vya maji ili kuepukana na changamoto ya ukame nchini.
Ameyasema hayo mkoani Morogoro alipotembelea banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu katika maonesho ya 30 ya Kanda ya Mashariki.
Kwa upande wake mtaalam wa maji juu ya ardhi magreth path amesema lengo la Bodi ya maji Bonde la Wami Ruvu ni kutunza na kuhifadhi rasilimali za maji pamoja na kupanda miti kando za mito..