Home MICHEZO JADON SANCHO AMJIA JUU KOCHA WAKE KWA KUMUWEKA BENCHI

JADON SANCHO AMJIA JUU KOCHA WAKE KWA KUMUWEKA BENCHI

 

Na Dishon Linus

Kocha mkuu wa Manchester United Erik Ten Hag amesema sababu ya Jadon Sancho kutokuwa sehemu ya kikosi kilichoikabili Arsenal hakufanya vizuri katika uwanja wa mazoezi.

Baada ya taarifa hii kutoka Jadon amesema watu hawapaswi kuamini kila kinachosemwa, kama ni mazoezini ameonyesha kiwango bora labda kama kuna sababu nyingine iliyomfanya kocha asimjumuishe na sio kiwango cha Mazoezini.

Jadon amesema yeye alikuwa tayari kuipigania timu yake kwa furaha na amani lakini alishangaa kuona hayupo sehemu ya kikosi kilichoikabili Arsenal.

Kabla ya kufungwa magoli 3-1 dhidi ya #Arsenal, Ten Hag alisema Sancho hajaonesha kiwango kizuri mazoezini ndio maana hakuwepo katika mipango yake

Baada ya mchezo huo, Sancho (23) akasema “Nimeonesha bidii mazoezini wiki hii, naamini kuna sababu nyingine ambazo siwezi kuzizungumza. Nimekuwa ‘mbuzi wa kafara’ kwa muda mrefu, sio haki.”

Previous articleSERIKALI YATOA MAJIBU KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA LAMI MLIMBA
Next articleWATENDAJI WIZARA YA UJENZI WATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU NA UADILIFU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here