Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kutinga fanali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ( UEFA Champion league),mara baada ya kutamatika kwa mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ampambo Inter Milan imeibuka mshindi mbele ya wahasimu wao Ac Milan 0 vs 1 Inter Milan na hivyo kufanya ushindi jumla kusomeka Inter Milan 3 vs 0 Ac Milan (Aggregate).
Mchezo huo wa marudiano uliochezwa katika dimba la San Sirro ,uliwakutanisha watani wa jadi wa jiji la Milan,ambapo dabi hiyo inafahamika kama Debby Della Madonina
Inter Milan sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati Manchester City dhidi ya Real Madrid utakaochezwa leo katika dimba la Etihad ndani ya jiji la Manchester nchini Uingereza.
Mara ya mwisho kwa timu ya Inter Milan kutinga fainali ya UEFA ilikuwa ni mwaka 2010 ambapo Ilifanikiwa kutinga fainali mara baada ya kuitoa timu ya Fc Barcelona.