Home KITAIFA HUKUMU KESI YA BANDARI KUTOLEWA MWEZI UJAO

HUKUMU KESI YA BANDARI KUTOLEWA MWEZI UJAO

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kupinga mkataba wa bandari Agosti 07, 2023 baada ya pande zote mbili za waleta maombi na wajibu maombi kumaliza kuwasilisha hoja zao.

Awali mawakili wa Serikali kwenye kesi hiyo ya kikatiba ya kupinga mkataba wa Bandari waliiomba Mahakama kutupilia mbali madai ya waleta maombi kwa maelezo kuwa mkataba wa kimataifa kati ya Tanzania na Dubai haujavunja katiba ya nchi.

Wakili mkuu wa Serikali Mark Mulwambo aliomba wapatiwe gharama za uendeshaji shauri hilo kwani waleta maombi hawakuwa na kesi ya msingi ya kuwasilisha mahakamani.

Naye wakili wa Serikali Edwin Webiro amesema ibara ya nane inasema Serikali itahakikisha haki mkataba hauathiriki kwa mujibu wa sheria lakini mwekezaji au raia wa kigeni haruhusiwi kumiliki ardhi ya Tanzania so sio kweli kwamba Dp World amepewa au atapewa sehemu yabardhi yetu.

Akijibu hoja hizo Wakili wa kujitegemea Livino Ngalimitumba, ameiambia Mahakama leo itazame kwa umakini uhai na ulinzi wa raslimali za Taifa badala ya kujikita kwenye ardhi pekee kwani hata mkataba wa DP World hautakuwa na fursa za ajira, uangalizi wa usalama wa wa-Tanzania mahala pa kazi OSHA, Shirika la viwango Tanzania TBS wala Wakala wa Bandari Tanzania TPA kama ambavyo Serikali inajinasibu kuwa mkataba huo utakuwa na fursa hizo.

Wakili Ngalimitumba, amesema endapo Tanzania itaona mkataba wa Bandari kati yake na kampuni ya Dp World hauna maslahi na ikataka kuuvunja haitawezekana isipokuwa kwa ridhaa ya Dubai na kwamba mkataba huo hauruhusiwi kuvunjwa wala kusitishwa hivyo kudai ni mkataba tata na kuiomba mahakama kuangazia zaidi kwenye maamuzi yake juu ya raslimali hizo za nchi zitakavyolindwa kwa mujibu wa sheria.

Majaji watatu wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya chini ya Mwenyekiti wa jopo hilo Jaji Dustan Ndunguru, wameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 07, 2023 kesi itakapokuja kwa ajili ya kutolewa kwa maamuzi ambapo jaji Nduguru amewashukuru mawakili wa pande zote mbili.

Previous articleDUWASA KUTUMIA ZAIDI YA BIL. 30 KUTEKELEZA MIRADI MINNE YA UCHIMBAJI VISIMA
Next articleNIRC KUJENGA MABWAWA 100 NCHI NZIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here