Home KITAIFA HAZINA SACCOS YATOA VITI MWENDO 15 BMH

HAZINA SACCOS YATOA VITI MWENDO 15 BMH

Chama cha Akiba na mikopo cha Hazina (HAZINA SACCOS) leo Disemba 8, imetoa msaada wa Viti mwendo (wheelchair) 15 vyenye thamani ya 5m/- kwa ajili ya kusaidia wagonjwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Akipokea msaada huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dkt Kessy Shija, amesema viti hivyo vitasaidia shughuli za kubeba wagonjwa wasioweza kutembea.

“Msaada huu wa viti mwendo utasaidia wagonjwa wasiojiweza kutembea na wazee wanapokuja BMH kupata huduma,” amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali.

Aidha, Dkt Shija ameishukuru Hazina SACCOS kwa msaada huo, akishauri taasisi nyingine kuiga mfano Hazina SACCOS wa kuwajali wananchi wengine hasa wanaokabiliwa na maradhi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Hazina SACCOS, Ndg Festo Mwaipaja, amesema wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kurudisha kwa jamii.

“Kwa kuwa, BMH ni moja ya wateja wetu na tunatambua huduma wanayotoa tumeona tuwapatie viti mwendo kwa ajili ya kusaidia huduma,” amesema Mtendaji Mkuu wa Hazina SACCOS.

Ndg Stanley Mhapa, moja kati ya wateja wa BMH, amesema msaada huo utawasaidia sana wagonjwa wanaokuja kupata huduma BMH hasa wasiojiweza kutembea.

“Viti mwendo vitasaidia hasa wazee wanapokuja kupata huduma hapa Hospitali na wagonjwa wasiojiweza kutembea kutoka kutoka Idara moja mpaka nyingine hapa BMH,” alisema Ndg Mhapa, ambaye ni mkazi wa Ilazo, jijini Dodoma.

Previous articleMWALIMU MAGANGA : NINA AJIRA YA KUDUMU CWT
Next articleDC ILEJE AMBANA MHANDISI KUTOKAMILIKA KWA ZAHANATI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here