Home KITAIFA HAKUNA VIFO WALA WAGONJWA WAPYA WALIOPATIKANA NA UGONJWA WA MARBURG

HAKUNA VIFO WALA WAGONJWA WAPYA WALIOPATIKANA NA UGONJWA WA MARBURG

 

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema muenendo wa Ugonjwa wa MARBURG uliozuka hivi karibuni Wilaya ya Bukoba, Vijijini, Mkoani Kagera hakujapatikana Wagonjwa wapya wala vifo na tayari mgonjwa mmoja amesharuhisiwa akiwa amehimarika Afya.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hadi kufikia Mwezi Aprili 2023 jumla ya watu 212 walitangamana na Wagonjwa kati ya 35 wamemaliza siku 21 za uangalizi za uangalizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa huo, hivyo wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kuungana na familia.

 

“Jumla ya visa 8 na kati yao watu 5 wamefariki ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa hatujapata Wagonjwa wapya wala vifo ninayo furaha kubwa kuwajulisha kues leo tumemruhusu mgonjwa mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 26 akiwa na afya njema”amesema Ummy.

 

Sanjari na hayo aliendelea kufanya kuwa Wagonjwa wawili walilazwa wanaendelea vizuri na matibabu katika vituo maalum vilivyoandaliwa hivyo serikali inatoa Shumrani za pekee Kwa Wataalamu wote wa afya waliokuwa mstari wa mbele kutoa huduma bora kwa Wagonjwa usiku na mchana kuhakikisha afya zao zinatengamaa.

 

Aidha Serikali inaendelea kuhimiza wananchi wote na hasa wa Mkoa wa Kagera kuendelea kuchukua tahadhari kudhibiti ugonjwa na kuzuia maambukizi mpya katika Jamii na endapo kutakuwa na mtu yeyote kwenye Jamii mwenye dalili za homa kali ikiwemo kutapika ,kuharisha ,kutokwa damu na mwili kuishiwa nguvu atoe taarifa haraka kwa kupiga simu 199 bila gharama zozote Ili apatiwe msaada wa haraka

Previous articleDITOPILE AGAWA FUTARI KONDOA, ASISITIZA KUIOMBEA NCHI NA KUMUOMBEA RAIS SAMIA
Next articleTAWOMA YASIFU MABADILIKO YA STAMICO KAMA MLEZI WA WACHIMBAJI WADOGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here