Na Joel Maduka Geita..
Utafiti ambao umefanywa na shirika liliso la kiserikali la Hakirasilimali kwa Mikoa ya Mara na Geita imebaini bado kunashida kwa makampuni ya uchimbaji wa madini kuchelewesha malipo Kwa wajasiliamali na wafanyabiashara wanaotoa Huduma katika migodi hali ambayo inachangia kuzorotesha mzunguko wa Biashara kwa wajasiliamali pamoja na kuishiwa mitaji ya kuendeleza biashara zao.
Hayo yamebainika mapema leo kwenye warsha ya siku moja iliyofanyika Mkoani Geita ambapo Afisa ufuatiliaji,Tathimini na mafunzo Kutoka Hakirasilimali Francis Mkasiwa amesema kuhusu Hali ya ajira Kwa wazawa Utafiti unaonyesha kuwa wazawa wanapewa kazi za kuuza mbogamboga,Huduma za usafiri,malazi,kuuza Chakula na kuuza vifaa vya ujenzi.
“Lakini bado utafiti wetu umeonesha wale watu ambao wanatoa huduma kwenye migodi wengi wao wamedai wanacheleweshewa malipo kwa Hali inayokwamisha mzunguko wa Biashara zao pamoja na kuishiwa mitaji Yao”Francis Mkasiwa Afisa ufuatiliaji ,Tathimini na mafunzo kutoka Hakirasimali.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mtandao wa mashirika yanayofanya kazi katika sekta ya madini na Gesi (Hakirasilimali) Jimmy Luhende amependekeza kuendelea kufanyika tafiti nyingi za kisayansi katika migodi inayozunguka wananchi ili kunufaisha pande zote za wawekezaji na wananchi.
“Ni ukweli nyuma kulikuwa na changamoto ya wazawa kupewa udhabuni kwenye maeneo yetu ya migodi mikubwa lakini kwa sasa tunashukuru kuwa sharia imesaidia kwa kiasi kikubwa ingawa bado tunatamani kuona wanawake pia wanapatiwa tenda hizi hili waweze kujikimu kimaisha na tunaamini kuwa serikali ikisaidiana na wadau wa maendeleo kama itafanya utafiti wa wapi wanawake wanakwama kupata tenda itasaidia zaidi kujua na mwisho wa siku kuwainua pia wapate tenda”Jimmy Luhende Mwenyekiti wa Bodi Hakirasilimali.
Shakira Said ni mkazi wa Geita amesema bado wanawake wanapitia changamoto kubwa ya ushirikishwaji katika Sekta ya madini kutokana na kunyimwa nafasi ambayo chanzo chake kikubwa ni kukosekana kwa mitaji mikubwa ambayo inaweza kuwasaidia kupata tenda kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini.
Warsha hiyo ya Siku moja iliyofanyika Mkoani Geita ya uzinduzi wa ripoti ya Utafiti wa Ushirikikishwaji wa wazawa Kwenye sekta ya madini iliyoandaliwa na Hakirasilimali na Policy Forum imejumuisha wadau wa madini Kutoka mkoa wa Mara,Shinyanga na Geita.