Home KITAIFA GF TRUCKS & EQUIPMENT YAIBUKA MSHINDI MAONYESHO YA MADINI RUANGWA

GF TRUCKS & EQUIPMENT YAIBUKA MSHINDI MAONYESHO YA MADINI RUANGWA

 

Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd ya jijini Dar es Salam imeibuka mshindi wa Pili wa Banda Bora kwa makampuni yanayotoa huduma ya uuzaji wa mitambo na magari Migodini.

Hayo yamebainika wakati wa kuhitimisha Maonyesho ya Madini na Uwekezaji yaliofanyika Rwangwa mkoani Lindi yalioanza tarehe 21 na kuhitimishwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliye ambatanana na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambae alikua mgeni Rasmi

Akizungumza wakati wa ufungaji wa Maonyesho hayo Kikwete alisema Wakati anastaafu aliiacha Rwangwa ikiwa haikuwa hivi na amekuja ameikuta Rwangwa ile na hii ya sasa ni Mbingu na ardhi kutokana na uwekezaji wa madini na fursa zilizopo mkoa wa Lindi kwenye Madini hivyo mabadiliko ni makubwa mno.

Nae Afisa Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Peter William alisema wao kama Gf wamejikita kuhakikisha wanawakomboa wachimbaji wa dogo na wakati kwa kuanzisha mapango maalumu wa kuhaikisha wanawawezesha wachimbaji nchini kupata mitambo ya kuchimbia kwa gharama nafuu kwa kushirikiana na taasisi za Kibenki wameazisha utaratibu wa kumkopesha mashine (matambo )iki kuweza kufanya kazi kwa uharaka Zaidi.


Pia Peter alisema wamejipanga kuwekeza nguvu Zaidi na hivi karibuni watafungua ofisi katika ukanda wa kusini ili wateja wasipate usumbufu wa kuja hadi Dar es salaam.
Kampuni ya Gf inayojishungulisha na uuzaji wa Magari ya FAW, FORLAND,HONG YANG (trucks) pamoja na mitambo ya XCMG maalumu kwa shuguli za migodini na Wakandarasi wa Barabara.

Akihitimisha maonyesho hayo Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa onyo kwa maafisa wanaohusika na utoaji wa leseni za madini kuacha tabia ya kuwazunguka wananchi wanaokwenda katika ofisi zao kuomba leseni za uchimbaji baada ya kubaini uwepo wa madini kwenye baadhi ya maeneo na kisha kuwapa wachimbaji wengine.

”…Acheni tabia ya kuwaonea wananchi wanaotoka kwenye maeneo yenye fursa ya madini anakuja kuomba leseni ya kumiliki eneo hilo na unamwambia aache taarifa zake aje kesho kuchukua majibu akija kesho unamwambia eneo hilo limeshachukuliwa na mtu mwingine kumbe wewe unamtafuta mtu wa kuweza kumiliki ili upate chochote kitu, tukikugundua hatua kali zitachukuliwa dhidi yako. ”

Ameyasema hayo (Jumamosi, Agosti 26, 2023) wakati akifunga Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji mkoani Lindi yaliyofanyika kwenye viwanja vya soko la Kilimahewa wilayani Ruangwa. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira bora kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania ufanye tafiti za madini za kimkakati kwa kushirikiana na halmashauri kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kufanya shughuli zao kwa tija na kuhakikisha mipango sahihi ya matumizi ya ardhi inafikiwa.

Previous articleSAMIA AWAWEKA MA- RC ‘ KITANZINI _ MAGAZETINI LEO JUMATATU AGOSTI 28/2023
Next articleDC SAME ATOA MWEZI MMOJA GULIO KUHAMISHWA 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here