Home MICHEZO FIFA YAANZA UCHUNGUZI KUHUSU TUKIO LA RAIS WA SOKA UHISPANIA KUMBUSU MCHEZAJI

FIFA YAANZA UCHUNGUZI KUHUSU TUKIO LA RAIS WA SOKA UHISPANIA KUMBUSU MCHEZAJI

 

Na Dishon linus

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limeanzisha uchunguzi dhidi ya rais wa shirikisho la soka nchini Uhispania Luis Rubiales baada ya kumbusu kiungo wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania Jennifer Heromoso kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uingereza katika fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake.

Hatua hii ya (FIFA) haishangazi hata kidogo kutokana na kile kilichotokea wakati wa kusherehekea kombe la Uhispania baada ya kushinda Kombe la Dunia. Wakati Hermoso, mfungaji wa bao pekee kwenye mchezo huo alipoenda kupokea medali yake ya dhahabu Rubiales alimbusu kwenye midomo jambo ambalo Hermoso hakuridhia nalo, kwani alisema “Sikupenda Kwa kile alichonifanyia”.

Ingawa ameomba msamaha tangu wakati huo, waziri mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, anaamini kwamba msamaha wake haukuwa wa kutosha. “Radhi zilizotolewa na Bw. Rubiales hazitoshi,hata nadhani hazifai na kwamba, kwa hivyo, Bw. Rubiales anahitaji kuendelea kuchukua hatua za kufafanua kile ambacho sote tuliona,” Sanchez alisema.

“Lakini ni kweli kumekuwa na tabia fulani, katika suala hili la bwana Rubiales jambo ambalo linaonyesha kuwa katika nchi yetu bado kuna safari ndefu katika suala la usawa na heshima na katika usawa huu wa haki kati ya wanawake na wanaume”.

Mbali na kauli za Sanchez kuhusu hali hiyo, Chama cha Wanasoka wa Uhispania (AFE) pia kilitoa taarifa “Ishara za kimwili zinazoelekezwa kwa mtu yeyote katika kesi hii mwanasoka kamwe hazifai au kukubalika katika muktadha wowote bila idhini ya moja kwa moja ya mtu aliyeathirika.”

Vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa Rubiales anakaribia kuwasilisha kujiuzulu kwake kutoka Shirikisho la Soka la Uhispania katika siku zijazo.

Previous articleEL NINO KUTIKISA NCHI KUANZIA OKTOBA – MAGAZETINI LEO IJUMAA AGOSTI 25/2023
Next articleMRADI WA UMEME WA JULIUS NYERERE WAFIKIA ASILIMIA 90.19

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here