Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania ( Femata ) imezindua semina ya uzinduzi wa mafunzo ya mradi wa vitambulisho vya Kidijitali kwa wachimbaji wa madini Tanzania lengo ikiwa kujua idadi ya wachimbaji wadogo ili kusaidia kuanzisha kanzidata.
Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania ( Femata ) John Bina amesema, vitambulisho vya wachimbaji wadogo wa madini kitawasaidia kuwatambua wachimbaji katika Taasisi za serikali ili waweze kukopesheka katika Benki kutokana na kutoaminika pia kutambulika katika uchimbaji sehemu yoyote ya Tanzania
Hivi vitambulisho tunafikilia kuvitumia katika uchaguzi na pia ndio iwe njia ya kupata wanachama na kwenye katiba moja ya vitu vilivyozungumzwa kuhakikisha Femata inatembea katika mstari mmoja hiki kitambulisho kinatolewa kuwa ni cha Femata lakini mwanachama awe amejiandikisha katika vyama vyao vya mikoa,John Bina” Mwenyekiti Femata.