Home KITAIFA FATAKI NA BARUTI ZAPIGWA MARUFUKU UWANJANI MECHI KATI YANGA NA MARUMO...

FATAKI NA BARUTI ZAPIGWA MARUFUKU UWANJANI MECHI KATI YANGA NA MARUMO GALLANTS

 

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatambua kuwa Jumatano tarehe 10 Mei, 2023 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam kutakuwa na mchezo wa soka Kombe la Shirikisho Afrika baina ya klabu ya Yanga na Marumo Gallants ya Afrika Kusini
utakaochezwa kuanzia saa 10:00 jioni.

 

Kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam tayari linachukua
tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo. Usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu maeneo yote ya kuzunguka uwanja ndani, nje na barabarani.

 

Hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote , isipokuwa baadhi ya
vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo.

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye
tabia ya kuwasha fataki na baruti uwanjani, kurusha chupa au kitu chochote. Hayo ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka.

Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo ambazo zimeanza kuzoeleka, na watakofanya,
watakamatwa wakati huo au baada ya mchezo kutegemea mazingira ya eneo mtuhumiwa
huyo atakapokuwa na watachukuliwa hatua za kisheria.

Muliro J. MULIRO – SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Previous articleDKT. DUGANGE HAJAJIUZULU NI UZUSHI UPUUZWE
Next articleRAIS SAMIA AMTEUA BISANDA KUWA M/KITI WA TUME YA TAIFA YA UNESCO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here