Home KITAIFA DP WORLD YAWAINUA VIONGOZI WA DINI WATAKA MJADALA WA AMANI.

DP WORLD YAWAINUA VIONGOZI WA DINI WATAKA MJADALA WA AMANI.

Rais wa manabii na mitume Tanzania Nabii Joshua amewataka watanzania kua watulivu wakati serikali inaendelea na mchakato wa mkataba wa bandari na kampuni ya DP World .

Nabii Joshua ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro ambapo amesema hapingi watu wanavyotoa maoni kuhusu mchakato wa mkataba lakini namna ya uwasilishaji maoni baadhi ya watu umekua tofauti kwa matumizi ya lugha kwa viongozi serikalini jambo ambalo linaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Anasema kama kiongozi wa dini anawajibu wa kuwakumbusha watu suala la utuzaji amani hivyo anaomba mjadala uwe mzuri kuzingatia matumizi ya lugha kwa viongozi ili waendele kuleta majibu yenye ufanisi kwa wananchi wao.

Nabii Joshua anasema tayari viongozi mbalimbali wa serikali wameshatolewa ufafanuzi baadhi ya mambo ambayo yamekua mjadala kwa wananchi hivyo njia rahisi ya uwasilishaji maoni ni kutumia mamlaka husika ili waweze kuyafanyia kazi badala ya kutumia mitandao kutoa lugha zisizo za stara

Anasema anatambua lengo la serikali ni kuwaletea maendeleo wananchi hivyo wananchi waendelee kuiamini pamoja na kuwaamini viongozi kwa ujumla ili taifa liweze kunufaika na mikataba mbalimbali ya uwekezaji iliyopo nchini

Aidha ameiomba serikali kutopuuza maoni ya wananchi badala yake wasikilizwe na yafanyiwe kazi ili kiu na matamanio yao yaweze kupata majibu yaliyosahihi kwa maslahi mapana ya taifa kwa ujumla

Previous articleMWANZA YAPOKEA MWENGE WA UHURU, KUKIMBIZWA KWENYE MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 21
Next articleWITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUTUMIA NISHATI YA UMEME, KUBUNI MIRADI YA KUJIONGEZEA KIPATO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here