Home KITAIFA DODOMA JIJI FC WAENDELE KIJIFUA MKOANI IRINGA

DODOMA JIJI FC WAENDELE KIJIFUA MKOANI IRINGA

Na Dishon Linus

Kikosi Cha Dodoma jiji FC kimeendelea na mazoezi ya kujiwinda kuelekea msimu mpya wa 2023/2024 NBC PL mkoani Iringa ikiwa leo wamecheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Kipigwe FC.

Katika mchezo huo ambao wamefanikiwa kushinda kwa goli 5 kwa 1 kikosi Dodoma jiji kimeimarika na kuweza kucheza mchezo wao wa kwanza na kuweza kufanikiwa kushinda hii leo.

Kocha msaidizi wa Dodoma jiji amesema “mchezo wetu wa kwanza kucheza wa kirafiki na timu kutoka hapa mkoani Iringa tumefanikiwa kushinda lakini ni wapongeze wapinzani kwa kuweza kutuonesha mchezo mzuri wa kujipima”.

Kocha huyo Kassimu Lyogope amesema pia wanatarajia kupata mchezo mwingine wa kirafiki siku mbili mbele kabla ya kutafuta timu ya ligi kuu ili kuweza kupata uwezo sawa ili tu kijiweka vizuri na msimu mpya wa ligi

Dodoma jiji wameweka kambi mkoani Iringa na mzoezi yao wakiyafanya katika uwanja wa Samora asubuhi na jioni kwa wiki tatu

Previous articleDC, MALISA, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA KIJIJI CHA SHAMWENGO NA KUZIPATIA MAJIBU
Next articleSERIKALI YAONDOA MAPINGAMIZI KESI YA BANDARI, MAHAKAMA KUU KUAMUA NI MKATABA AMA LAA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here