Home KITAIFA DKT. YONAZI “TUTAENDELEA KUELIMISHA UMMA MASUALA YA MAAFA”

DKT. YONAZI “TUTAENDELEA KUELIMISHA UMMA MASUALA YA MAAFA”

NA. MWANDIZI WETU

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kupitia Idara ya menejimenti ya maaafa imesema itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na majanga mbalimbali pindi yanapotokea ili kupunguza athari za majanga hayo.

Akizungumza hii leo Julai 6, 2023 wakati alipotembelea maonesho ya kimataifa ya 47 ya biashara maarufu kama sabasaba Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Serikali inaendelea Kushirikiana na wadau ili kuhakikisha kuwa uwezo wa nchi katika kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea unaboreshwa.

Aliongezea kuwa, Serikali itaendelea kuratibu vyema masuala ya menejimenti ya maafa kwa kuzingatia mifumo ya kitehama ili kuwafikia wananchi kwa wakati kuendelea kuleta matokeo yanayokusudiwa.

“Serikali imewekeza katika mifumo mbalimbali ya kiteknolojia inayosaidia kutoa Viashiria vya awali vya majanga na pia kusaidia katika utoaji wa taarifa kwa haraka,”Alieleza Dkt. Yonazi.

Pia akieleza mikakati ya serikali kuratibu masuala ya maafa alisema imejipanga kuufikia umma wa Watanzania kuanzai ngazi ya Kijiji, Kata, Wilaya , Mkoa hadi Taifa na kwa kuzijengea uwezo kamati za maafa kwa ngazi zote na kuwa na jamii stahimilivu ya maafa nchini.

“Katika mwaka huu mpya wa fedha, tumejipanga kuendelea kujenga uwezo kwa wadau wetu ili kuhakikisha uwezo wetu wa kukabiliana na majanga aina mbalimbali unaboreshwa kwa kuzingatia athari zake kiuchumi, kijamii na nyingine nyingi,” Alisisitiza Dkt. Yonazi

Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO APOKEA VIFAA TIBA VYA WATOTO NJITI BUHIGWE
Next articleBEI YA SUKARI YAPAA DUKANI, BODI YAKANA KUHUSIKA NAYO_ MAGAZETINI LEO IJUMAA JULAI 07/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here