Home KITAIFA DKT. SHEKALAGE, DKT. JINGU WAKABIDHIANA OFISI RASMI

DKT. SHEKALAGE, DKT. JINGU WAKABIDHIANA OFISI RASMI

 

Na WMJJWM, DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekhalage amewasili katika ofisi yake mpya na kukabidhiwa Ofisi hiyo na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. John JinguĀ  Septemba 4,2023.

Tukio hilo ni kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyohusisha Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu hivi karibuni.

Akizungumza na Menejimenti ya Wizara mara baada ya makabidhiano, Dkt. Shekhalage ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana ili kufikia lengo la kuwahudumia Wananchi.

“Nitakuwa tayari kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri, niwahakikishie kuwa mimi nitakuwa mtumishi mwenzenu, tutafanya kazi kwa umoja na ushirikiano”

Kwa upande wake Dkt. Jingu ameishukuru Menejimenti na watumishi kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote alichofanya kazi Wizarani hapo.

Naye Waziri Mhe. Dkt Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi, amesema lengo la Mheshimiwa Rais kufanya mabadiliko hayo ni jema ili kuendelea kuwatumikia watanzania.

Amemshukuru Dkt. Jingu kwa utendaji wake akiwa Wizarani hapo na kumtaka ashirikiane vozuri na Katibu Mkuu Dkt. Shekhalage katika utendaji kwani Wizara hizo zinategemeana.

“Wizara ya Maendeleo ya Jamii ikifanya vizuri kwenye Jamii,hata kwenye Hospitali zetu wagonjwa watapungua” amefafanua Waziri Dkt. Gwajima.

Previous articleVITUO VYA MAFUTA VYAFUNGIWA , KASHFA YA KUFICHA MAFUTA_ MAGAZETINI LEO JUMANNE SEPTEMBA 05/2023
Next articleAWESO ASISITIZA KUPATA MAJIBU NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA MAJI KWA WAKATI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here