Home KITAIFA DKT. MWINYI AHIMIZA UMOJA KWA WANA-CCM ZANZIBAR, AAGIZA KAMATI ZA MAADILI KUFANYA...

DKT. MWINYI AHIMIZA UMOJA KWA WANA-CCM ZANZIBAR, AAGIZA KAMATI ZA MAADILI KUFANYA KAZI ZAKE

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK. Hussein Ali Mwinyi amesema mara tu baada ya uchaguzi kumalizika, ni muhimu kwa Chama na Wanachama kujenga umoja, kwa kuondoa makundi yote na kushirikiana kwa pamoja.

 

Dk Mwinyi amewaasa wale ambao wanaendelea kukiuka taratibu na kuchangia kuwepo kwa makundi wanapaswa kuitwa na kuchukuliwa hatua na kamati za maadili ili kuhakikisha nidhamu na mshikamano ndani ya chama.

 

Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika mkutano wa viongozi wa CCM ngazi ya Shina , Majimbo , Wilaya na Mkoa katika ziara yake ya kukiimarisha chama na kutembelea miradi mbalimbali ukumbi wa Picadilly, Kombeni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Previous articleDC AAGIZA KILA KAYA KUFUGA KUKU WASIOPUNGUA WATANO
Next articleWAZIRI AWAONYA WANAWAKE JEURI, KUJIKWEZA KISA VYEO NA VIPATO _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI MEI /2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here