Home KITAIFA DKT. MPANGO HAKI ITOLEWE KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA

DKT. MPANGO HAKI ITOLEWE KWA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA

Makamu wa Rais Dkt .Philip Mpango amesema takwimu za January – Disemba 2022 zinaonesha matukio ya ukatili yamekuwa mengi zaidi ambapo ubakaji ni 6,335, ulawiti 1,555 na mimba za utoto 1,557. hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko ukatili wa kijinsia hapa nchini.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) kwa Mkoa wa Ruvuma.

Makamu wa Rais ametaka kampeni hiyo kusaidia waathirika wa vitendo hivyo kupata haki zao pamoja na kuagiza vyombo vya dola kuendelea kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya Watuhumiwa wote wa matukio hayo.

Kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Campaign) inatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Machi, 2023 hadi Februari, 2026 ikitarajiwa kuwafikia katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Mkoa wa Ruvuma ni Mkoa wa nne kuzindua kampeni hiyo ukitanguliwa na mikoa ya Dodoma, Manyara na Shinyanga.

Previous articleCHONGOLO KUWASHA MOTO SINGIDA LEO…YANGA SC YATUMA SALAMU NBC, CAF _ MAGAZETINI LEO JUMAPILI JULAI 23/2023
Next articleKINANA KUANZA ZIARA DODOMA, MANYARA, MARA, SIMIYU, TABORA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here