Home KIMATAIFA DKT. MPANGO ATUA NCHINI BURUNDI

DKT. MPANGO ATUA NCHINI BURUNDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akilakiwa na Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Mjini Bujumbura nchini Burundi, leo tarehe 06 Mei 2023.

Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano kwaajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Mjini Bujumbura nchini Burundi, leo tarehe 06 Mei 2023.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisalimia viongozi mbalimbali alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Mjini Bujumbura nchini Burundi, leo tarehe 06 Mei 2023. Kulia ni Mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza.
Previous articleSIMBACHAWENE AWATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UONGOZI, TMDA YAPONGEZWA
Next articleTEITI KUJA NA MPANGO MKAKATI WA KUWAKOMBOA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI TANZANIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here