Home KITAIFA DKT. MAGEMBE AKOSHWA NA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA

DKT. MAGEMBE AKOSHWA NA HUDUMA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA

 

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa jitihada kubwa zinazofanywa katika uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapa.

Akiongea baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Mbeya ameupongeza uongozi na watumishi kwa kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Nyanda za Juu Kusini.

“Niwapongeze pia kwa kazi nzuri mnayofanya, tunaona jinsi wananchi wanavyowapongeza lakini pia tunaona utayari na uharaka wenu tunapowaletea changamoto za wananchi huwa mnakuwa wepesi kuzitatua”, Dkt. Grace Magembe, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya.

Aidha amesisitizia uongozi wa hospitali kuwajengea uwezo wataalamu walio katika ngazi ya msingi kwa lengo la kuwaongezea ujuzi katika kutoa huduma bora.

“Pamoja na kazi zote mnazofanya bado mnakumu la kuzijengea uwezo Hospitali za Wilaya na vituo vyote vilivyoko katika ngazi ya msingi”, ameeleza Dkt. Grace Magembe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji ameishukuru Serikali kupitia wizara ya afya kwa uboreshaji wa wamiundombinu na vifaa tiba ikiwemo mashine ya MRI na kuhaidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Wizara ya afya kupitia Naibu Katibu mkuu Dkt. Grace Magembe.

“Tutaendelea kushirikiana na wenzetu, sisi kama Hospitali ya Kanda Mbeya, ni wajibu wetu kuwajengea uwezo Hospitali za Wilaya na ngazi ya msingi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora”, Dkt. Godlove Mbwanji.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo huduma za mionzi na Huduma za vipimo vya MRI pamoja na huduma za Afya ya Mama na Mtoto.

Previous articleWAZIRI JAFO AIAGIZA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KUIPA KAMPUNI YA GIVORAH KIBALI CHA KUCHUKUA TAKA DAMPO LA PUGU KINYAMWEZI NDANI YA SIKU 15
Next article“UWEKEZAJI WA DP WORLD NI HATUA ZA AWALI HATUJAINGIA MKATABA ZINAZOENDELA NI PROPAGANDA CHAFU” FATMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here