Home KITAIFA DKT. BITEKO ATETA NA KAMPUNI YA SOTTA MINING DODOMA

DKT. BITEKO ATETA NA KAMPUNI YA SOTTA MINING DODOMA

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko leo Agosti 3, 2023 jijini Dodoma amekutana na Uongozi wa Juu wa Kampuni ya Sotta Minerals Corporation Limited ambayo ni ya ubia Kati ya Serikali na kampuni ya Orecorp Tanzania limited ya Australia inayosimamia Mradi wa uchimbaji madini ya dhahabu uliopo wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Kupitia Mkutano huo, kampuni ya Sotta imeeleza maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka 2025.

Aidha, Dkt. Biteko ameelezwa kuwa, hivi sasa kampuni iko kwenye hatua za mwisho za kuweza kuwalipa fidia wananchi walio ndani ya eneo la mradi ili kuwezesha mradi huo kuanza.

Previous articleTANI 1500 ZA UFUTA ZAUZWA MKOANI PWANI, ZAINGIZA BILIONI 60
Next articleBANDARI YAMPELEKA MWANAHABARI KALULUNGA POLISI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here