Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa ziarani nchini Qatar, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi utakaofunguliwa kesho.
Katika ziara yake Rais Dk.Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar mhe.Muhamed bin Ahamed Al-Kuwari na wadau kutoka sekta binafsi ya viwanda.
Dk.Mwinyi amewakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuja kuwekeza Zanzibar kutokana na fursa zilizopo, pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni Utalii na kumbi za mikutano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Baraza la uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Shariff Ali Shariff alieleza fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar zaidi katika sekta ya Utalii hususani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kulingana na kuongezeka kwa soko la Utalii.