Home KITAIFA DC SAME ATOA MWEZI MMOJA GULIO KUHAMISHWA 

DC SAME ATOA MWEZI MMOJA GULIO KUHAMISHWA 

 

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni,ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhamisha gulio linalofanyika Jumatano hadi Jumapili eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanja vya michezo maarufu Kwasa-kwasa na kusababisha malalamiko kwa wanamichezo ambao wanashindwa kutumia eneo hilo.

Ameeleza pia kutoridhishwa na hali ya soko la mji wa Same kutokana na uchafu uliokithiri, vyoo vinavyotumika kukosa ubora unaohitajika hivyo kuhatarisha usalama wa wafanyabiashara na wananuzi wanaotumia soko hilo na kuagiza halmashauri kukarabati vyoo vinavyotumika sokoni hapo kufikia Septemba ya mwaka huu 2023.

Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko hilo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya ya Same ambapo amesisitiza uboreshwaji wa miundombinu kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara.

Awali wafabiabiashara wa soko kuu la mji wa Same wakitoa malalamiko yao wamemweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa soko hilo linakabiliwa na ubovu mkubwa wa miundombinu, uwepo wa mashimo makubwa yaliyo ndani ya soko pia kukosekana nishati ya umeme hali inayosababisha kuendesha biashara kwa shida wakitaharisha pia usalama wao.

Previous articleGF TRUCKS & EQUIPMENT YAIBUKA MSHINDI MAONYESHO YA MADINI RUANGWA
Next articleRWANDA YAINGIA MKATABA WA UTALII NA KLABU YA BAYERN MUNICH YA NCHINI UJERUMANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here