Home KITAIFA DC MKALIPA ADHAMIRIA KUIFANYA HAI YA KIJANI KWA KUPANDA MITI

DC MKALIPA ADHAMIRIA KUIFANYA HAI YA KIJANI KWA KUPANDA MITI

SERIKALI wilayani Hai mkoani Kilimanjaro imedhamiria kutekeleza agizo la kupanda miti milioni moja na lakitano (1,500,000) ili kuboresha mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Amiri Mkalipa ameeleza hayo wakati akiongoza zoezi la upandaji miti rafiki kwa mazingira kwaajili ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiwilaya kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi, kupanda miti pamoja na michezo.

 

Mkalipa alisema wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapanda miti na kuitunza ili iweze kukua kwa lengo la kuboresha mazingira na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo kukata miti,kuchoma misitu,na shughuli za kilimo maeneo ya vyanzo vya maji.

 

“Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa mazingira yanaboreshwa kwa kupanda miti ,kuitunza na ninyi wananchi hakikisheni kwenye maeneo yenu mnapanda miti ya aina tofauti ikiwemo ya matunda ambayo itasaidia kutunza mazingira pamoja kupata matunda, kwa Wilaya tuna dhamiria kupanda miti milioni moja na laki tano.”

 

“Leo tumepanda miti kwenye maeneo ya Kia,Shule ya Sekondari ya wavulana Lyamungo na Shule ya wasichana Machame ,niwatake wananchi na viongozi mliopo kwenye maeneo husika kuhakikisha kuwa miti hii inalindwa na kukuwa na kuwachukulia hatua kwa mtu yeyote atakayefanya uharibifu kwenye miti hii” alisema Mkalipa

 

Hata hivyo, Mkalipa aliwataka viongozi na wananchi kuacha tabia ya kuotesha miti kwa ajili ya kipindi cha matukio na badala yake watumie msimu wa mvua kupanda miti kwa wingi kwa maslahi ya vizazi vijavyo.

 

Awali akitoa taarifa za uoteshaji wa miti,afisa misitu wa Wilaya, Mbayani Mollel alisema kuwa wamekusudia kupanda miti milioni moja na laki tano kwenye maeneo ya wazi pamoja na kwenye taasisi za Serikali na zisizo za Serikali.

Previous articleMKOA WA MWANZA WAADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO KWA KUZINDUA KAMPENI YA UHIFADHI MAZINGIRA NA CHANJO
Next articleRC MALIMA AWAKUMBUSHA WATANZANIA KUENZI MUUNGANO KWA KUFANYA KAZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here