Home KITAIFA DC MGOMI: WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI NYINYI NI INJINI ZA SERIKALI

DC MGOMI: WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI NYINYI NI INJINI ZA SERIKALI

Maafisa watendaji kata na vijiji wilayani Ileje wametakiwa kusimamia vyema utekelezaji wa mipango ya serikali kutokana na ukaribu wao na wananchi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi kwenye kikao cha tathimini ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi
yake.

Akizungumzia hali ya lishe ilivyoboreshwa kwa idadi ya shule zinazotoa chakula cha mchana kwa wanafunzi alisema, kumekuwa na mabadiliko makubwa hali inayoonesha kuwa viongozi hao wametimiza wajibu wao.

Mgomi amesema kuwa, serikali inawategemea sana watendaji hao ikiamini kuwa wana uwezo wa kushirikisha makundi mbalimbali ya kijamii katika kuwahudumia wananchi

Previous articleEWURA: NCHI INA MAFUTA YA KUTOSHA NA MELI ZENYE SHEHENA YA MAFUTA ZINAENDELEA KUINGIA NCHINI
Next articleEWURA YATOA ONYO KWA KAMPUNI ZINAZOFICHA MAFUTA _ MAGAZETINI LEO JUMANNE JULAI 18/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here