NA DENIS SINKONDE, SONGWE.
Taasisi za serikali wilayani Ileje mkoani Songwe zimeagizwa kushirikiana na taasisi binasfi zilizosajiliwa kisheria kwa lengo la kusaidia wanajamii wilayani humo kwenye nyanja mbalimbali.
Agizo hilo limetolewa na na mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi Juni 21,2023 wakati akizungumza na baadhi ya mashirika wakati yakiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya mwaka kuanzia Januari_ Disemba mwaka 2022 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya.
Mhe. Mgomi amesema, kuwa mashirika hayo yapo kwa mujibu wa sheria hivyo ngazi zote za uongozi hazina budi kutoa ushirikiano wa kutosha kwani yana mchango kwa serikàli katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mhe. Mgomi amesema, kuanzia ngazi ya vitongoji mpaka wilayani kiongozi atakayebainika haoneshi ushirikiano kwa mashirika hayo hata kama ni mtendaji wa kijiji, mpaka wakuu wa idara tutawashughulikia
“Tumeona mchango mkubwa sana wa mashirika haya kwa wananchi kusaidia kutoa elimu ya lishe, afya, kilimo, na ufugaji hivyo tuendelee kuwapa morali ya kwenye jamii”, amesema Mhe. Mgomi.
Niwaagize nanyi viongozi wa mashirika hakikisheni mnatekeleza majukumu yenu kama mlivyosajiliwa na kama mtafanya kazi nje na makubaliano yaliyopo kwenye sheria namba 24 ya mwaka 2022 hatutakuwa tayari kufanya na ninyi kazi.
Afisa kilimo kutoka shirika la HRNS Lizedi Cope amesema lengo la kusajiliwa ni kuisaidia jamii ya Ileje kwenye masuala mbalimbali ikiwepo kutoa elimu ya kilimo cha kisasa, kupambana na udumavu, ufugaji pamoja na afya Kwa lengo la kuwa na jamii yenye ustawi.
Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho ni HRNS, IRDO, HIMSO, PARALIGO, PAMOJA TUWAWEZESHE WANAWAKE, TACRI, SHALOOM na ADP MBOZI ambao kwa sehemu kubwa wamekuwa chachu ya maendeleo wilayani humo.