Home KITAIFA DC MBEYA AWATAKA WAHITIMU KADA YA AFYA KUITUMIKIA JAMII KWA UPENDO NA...

DC MBEYA AWATAKA WAHITIMU KADA YA AFYA KUITUMIKIA JAMII KWA UPENDO NA UZALENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewataka wahitimu wa chuo cha Afya K’S kilichopo jiji la Mbeya kwenda kuitumikia jamii kwa uzalendo na upendo kwani serikali ya awamu ya sita imewekeza zaidi kwenye huduma bora za afya nchini.

Akizungumza kwenye mahafali ya nane ya chuo hiko Mhe. Malisa amewakumbusha wajibu wao kama wataalam wa afya ya kuwa jamii inawahitaji hivyo ni vyema kutumia lugha za upendo katika kuwahudumia wagonjwa.

Kwa upande wake Norbert Sizari ambaye ni Mkuu wa Chuo hiko ameishukuru serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuwapa ushirikiano wanafunzi kwa kupata mafunzo kwa vitendo.

Previous articleTABASAM CUP 2023 YAZINDULIWA KUSHIRIKISHA TIMU 184
Next articleDARASA LA KWANZA HADI LA TATU WAANZE KUSOMA SHULE HII MPYA BADALA YA KUSUBIRI HADI JAN MWAKANI – ULEGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here