Home KITAIFA DC MBEYA AWAOMBA WATANZANIA KULIOMBEA TAIFA

DC MBEYA AWAOMBA WATANZANIA KULIOMBEA TAIFA

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Beno Malisa leo Jumapili ameshiriki ibada katika kanisala la ASSEMBLESS OF GOD GOSPEL CHURCH INTERNATIONAL lililopo kata ya Ruanda.

 

Mara baada ya kukaribishwa kuzungumza na waumini wa kanisa hilo ameliwaomba kuliombea taifa la Tanzania na viongozi wake, Mh Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, afya, hekima na uvumilivu na baraka katika majukumu ya kuongoza Nchi yetu, viongozi wasaidizi wake, Mkuu wetu wa Mkoa wa Mbeya Mh Juma Zuberi Homera pamoja na Mh Mbunge Dkt Tulia.

Katika kulifanya jiji kuwa Safi Mkuu wa wilaya amutumia muda huo na kuwahimiza Wananchi juu ya Suala la Usafi wa mazingira

 

Naye Askofu wa Kanisa hilo Dkt. Asumwisye Mwaisabila amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa Kuleta miradi mikubwa Mbeya Ambapo imekuja kuibadilisha Mkoa kwa kiasi kikubwa.

 

Aidha Mkuu wa Wilaya Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini kukemea vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Ameongeza kuwa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameleta Miradi mikubwa ya maendeleo Mbeya ikiwemo Ujenzi wa Barabara nne na Mradi wa Maji wa Mto Kiwira

Kanisa hilo limefanya maombi maalumu juu ya Rais Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake

Previous articlePOLISI YAANZA UCHUNGUZI MADAI YA MTOTO ALIYEKUFA NA KUZIKWA KISHA KUDAIWA KUONEKANA AKIWA HAI
Next articleMABINTI SONGWE WANAOGOPA SINDANO ZA CHANJO_ MAGAZETINI LEO JUMATATU MEI 01 /2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here