Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Shamwengo kata ya Inyala halmashauri ya wilaya Mbeya na kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzipatia majibu yake.
Katika mkutano huo Mhe. Malisa aliambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mhe. Mwalingo Kisemba, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Ndug: Stephen Katemba pamoja na wataalam mbalimbali.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Malisa amewahamasisha wananchi hao kujitokeza kwa wingi siku ya mkesha wa mwenge wa uhuru unaotarajia kufika September 10 mwaka huu na kukesha katika kijiji cha Inyala.
Hatahivyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Ndug: Stephen Edward Katemba amewahakikishia wananchi hao kuwa ifikapo July 28 mwaka huu zahanati ya Shamwengo itaanza kazi rasmi na kwamba kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji nayo imeanza kushughulikiwa.