Mkuu wa wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Kalist Lazaro amesema migogoro mingi inayotokea kati ya kijiji na kijiji au kata kwa kata inatokana na maslahi binafsi ya viongozi wa maeneo husika baada ya kuibuka kwa fursa mbalimbali za kiuchumi.
Hayo ameyasema baada ya kuwasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 / 2025 kwa wilaya ya lushoto.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kulingana na migogoro hiyo ya wilaya mbili watahakikisha wanaitatua kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya korogwe Joketi Mwegelo.