Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo amewapongeza akina mama wanaozalisha mbegu za asili za mazao mbalimbali ya chakula, matunda na mbogamboga.
Akina mama hao waonafanya shughuli za uzalishaji wa mbegu hizo chini ya mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), ambapo licha ya pongezi amewaalika kufika wilayani Korogwe ili kuwashirikisha wanawake wengine wilayani humo mbinu za uzalishaji.
Kwa upande wake afisa programu sera ujenzi wa nguvu za moja (TGNP )Rogathe Loakaki amesema,gharama ya uendeshaji wa shughuli za kilimo na viuatilifu ndivyo vimewasukuma kujikita katika kilimo cha mbegu za asili, ambapo kwasasa wameifikia Mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro na Manyara.