Home KITAIFA DC JOKATE AKABIDHI NYUMBA 8 KWA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA HATARISHI

DC JOKATE AKABIDHI NYUMBA 8 KWA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA HATARISHI

 

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Jokate Mwegelo amekabidhi nyumba nane kwa Watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi zenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 50.

Nyumba hizo zimejengwa kwa ufadhili wa pamoja kati ya Kanisa la Anglican Msambiazi pamoja na KKKT Emao Old Korogwe ikiwa na lengo la kuwanufaisha watoto hao kutoka katika wimbi la umasikini.

DC Jokate amesema “Rai yangu kwa hawa waliopatiwa nyumba hizi nane wasije wakatumia nyumba hizi kwa kuziuza au kupangisha kwanza ifahamike nyumba hizi ni za hawa Watoto kwahiyo Wazazi wanakaa kama Walezi tu wa kuwasaidia kuzishika lakini kwenye zile hati za makabidhiano majina yaliopo ni ya Watoto husika “

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hizo Mratibu wa Kituo cha Watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi Anglican Msimbazi Mery Msendekwa amesema kuwa Kanisa la KKKT EMAO limejenga nyumba nne na Anglican Msambiazi limejenga nyumba nne huku zote zikiwa na thamani ya Tsh. milioni 50.4

Mchungaji na Mlezi wa kituo cha Anglican Msimbazi Canon Jackson Matunga amesema lengo ni kuwawezesha Watoto hao kuishi mazingira mazuri na nyumba hizo ni mali za Watoto na endapo Mtoto atanyanyaswa kupitia nyumba hizo Kanisa litasimama na kuhakikisha watoto hao wanapata haki zao.

Previous articleORYX GASI YATOA MITUNGI 500 NA MAJIKO YAKE KWA MAMA LISHE JIMBONI KWA WAZIRI MABULA
Next articleTABASAM CUP 2023 YAZINDULIWA KUSHIRIKISHA TIMU 184

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here