Home KITAIFA DC ILEJE, TANROADS WAFANYA KIKAO, WANANCHI KUANZA KULIPWA FIDIA

DC ILEJE, TANROADS WAFANYA KIKAO, WANANCHI KUANZA KULIPWA FIDIA

Mkuu wa wilaya ya Ileje Bi. Farida Mgomi ameongoza kikao kazi cha ofisi  yake na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa lengo la kuunda kamati ya usuluhishi wa malalamiko yatokanayo na fidia kwa ajili ya ujenzi wa barabara ndani ya Wilaya ya Ileje kutoka Isongole – Isoko ikiwa ni awamu ya kwanza ya ujenzi yenye urefu wa kilometa 52.414

Kiasi cha shilingi za Kitanzania 50,265,900.70 kimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia ya wananchi ambao barabara hiyo inapita katika maeneo yao.

Kikao hicho kimefanyika Septemba 18,2023 kwenye Ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Itumba-Ileje.

Sambamba na uundwaji wa Kamati hiyo, Wakala ya Barabara nchini Tanzania (TANROADS) unatarajia kuanza kutekeleza malipo kwa wahusika hao jumla ya 312 mnamo Septemba 19,2023.

Previous articleMWENYEKITI WA WACHIMBAJI WADOGO NYANG’HWALE ASISITIZA VIONGOZI WA DINI KULIOMBEA TAIFA
Next articleAMKATA MWENZA KOROMEO NAE AJIUA KWA KUJICHOMA KISU TUMBONI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here