Home KITAIFA DC ILEJE: MIRADI YA BOOST IJENGWE KWA VIWANGO VYA JUU NA THAMANI...

DC ILEJE: MIRADI YA BOOST IJENGWE KWA VIWANGO VYA JUU NA THAMANI YA FEDHA IONEKANE

NA DENIS SINKONDE, SONGWE.

Wenyeviti wa vijiji ,walimu wakuu na kamati zilizoundwa kusimamia miradi ya BOOST kwenye Shule za msingi kwenye maeneo yao wilayani Ileje mkoani Songwe zimetakiwa kushirikiana na wananchi kwa lengo la kumaliza miradi hiyo kwa wakati.

Akizungumza na baadhi ya viongozi , na wananchi hao wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi huo mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Farida Mgomi amewataka wananchi kujitolea nguvu zao kwenye miradi hiyo ili kuokoa gharama za fedha na kujenga mradi wa viwango.

Mhe. Mgomi amewataka wasimamizi wa mradi huo wakiwepo wahandisi wa Halmashauri kufika kila mda kwenye miradi ili kujihakikishia viwango vinavyotakiwa na si kufanya marekebisho wakati mradi umekamilika itakuwa ni kukwamisha nguvu kazi za wananchi.

“Katika miradi hii tunatakiwa kuijenga kwa viwango na thamani ya fedha ionekane kwani dhamira ya serikali ni kutaka miradi hii idumu kwa mda mrefu kwa lengo la mwanafunzi apate mazingira mazuri ya kujifunzia”, amesema Mgomi.

Mhe. Mgomi amewapongeza wananchi namna walivyoonyesha ushiriki wa awali kwenye uanzaji ujenzi, huku akiwataka wenyeviti wa vijiji kuhakikisha wanawashirikisha wananchi ipasavyo.

“Ninyi wenyeviti mmepokea miradi hii hivyo hamna budi kuisimamia na kuhakikisha inamalizika kwa wakati kwani ninyi ndio mnatakiwa kusimamia hilo fungu la fedha kwa kushirikiana na walimu wakuu wa hizi shule, pamoja na kamati zilizoundwa kwa ajili yah ii miradi”, amesema Mgomi.

Mkazi wa Ibaba Assa Mbembela amemuomba mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha anawapitishia cheki ya fedha zinapohitajika ili kununua kwa wakati vifaa vya ujenzi hususani vya viwandani ili kuondokana na changamoto zinazoweza pelekea kukwamisha mradi .

Previous articleWABUNGE WAALIKWA KUTEMBELEA MRADI WA EACOP
Next articleBAJETI YA ARDHI YAPITA KWA ‘MBINDE; MZOZO WAIBUKA_MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MEI 27/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here