Home KITAIFA DC ILEJE AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTUMIA MITANDAO KUTANGAZA BIASHARA ZAO

DC ILEJE AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTUMIA MITANDAO KUTANGAZA BIASHARA ZAO

NA DENIS SINKONDE, SONGWE.

Wajasiriamali wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao Kwa lengo la kupata wateja wenye uhitaji wa bidhaa zao.

Hayo yamesemwa Julai 9 ,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi wakati akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo wadogo katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo katika kikao kilichoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hiko wenye lengo la kuhamasisha vijana kufanya biashara zao kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali.

Mgomi amewataka vijana kufanya biashara kulingana na wakati uliopo kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia kufungua akaunti za mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram na Twitter ili kuhakikisha wanajipatia kipato kupitia mitandao.

Mgomi amewataka vijana kuendelea kujifunza namna ya kutumia teknolojia ya kufanya biashara kwenye maeneo yao sambamba na kuomba mikopo ya asilimia 10, Kwa vijana 4% ,wanawake 4% na makundi maalaumu 2% isiyo na riba kwenye halmashauri Ili kukuza mitaji ya biashara zao.

“Ninapozungumzia mikopo ombeni mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba ambayo inatolewa na halmashauri kwa vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu, na si mikopo umiza maarufu kama kausha damu ambayo inaweza kusababishia kukimbia familia na kuiacha kwenye matatizo,” amesema Mgomi.

Mgomi amewataka vijana kujiunga pia kwenye vyama vya wafanyabiasha ambako huandaliwa jukwaa la kuwasilisha changamoto kupitia sekta binafai zinazowakabili kwenye biashara zao na kuzipatia ufumbuzi.

“Mahusinao mazuri kati ya sekta binafsi na serikali kunasaidia kuchochea maendeleo na uchumi kwa wananchi kupitia biashara wakiwepo vijana ambao ndio nguvu kazi Kwa taifa ,amesema Mgomi.

Mgomi amewasihi vijana kujiunga na vyama vya wafanyabiashara Tanzania ambavyo ni vyama vya Wafanyabiashara kama TCCIA,Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) , TWCC kwani vimekuwa kinara katika majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi.

Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wilayani humo Diana Ngabo amesema lengo la kuandaa hafla hiyo ni kuyatambua aina ya makundi ya vijana na kuwasilisha changamoto zinazowakabili mbele ya mkuu wa wilaya Ili ziweze kutatuliwa.

“Kama vijana watambue serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inapokea kero zinazowakabili vijana wajasariamali zinazowakwamisha kujifungua kiuchumi hivyo ni muhimu kuziwasilisha kwa viongozi wa chama na serikali ili zitatuliwe,” amesema Diana.

Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Ileje Maoni Mbuba akizungumza katika kikao hicho amewasihi vijana kuwa wazalendo na waminifu kwenye biashara zao na kutosita kuwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo katika shughulizi zao za Kila siku ili zipatiwe ufumbuzi.

“Hafla ambayo imeandaliwa na jumuiya ya vijana wilayani hapo itasaidia ilani ya chama kutekelezwa Kwa kuhakikisha vijana wanapata mikopo itakayowainua kiuchumi,” amesema Mbuba.

Brown Kaduma ambaye ni mjasiriamali ameiomba halmashauri kuwatengenezea mazingira rafiki wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara ikiwepo kupewa elimu ya mlipakodi na kuondoa uhasama baina yao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kauli mbiu ya wilaya ya Ileje inasema USHIRIKIANO WETU NDIO MAENDELEO YETU

Previous articleNDEGE YA TANZANIA ILIYOKUWA IMESHIKILIWA UHOLANZI YAREJEA NCHINI_ MAGAZETINI LEO JUMATATU JULAI 10/2023
Next articleJUSSA: TUNATAKA RAIS ANAYEHESHIMU KATIBA NA UTAWALA WA SHERIA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here