Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Mhe. Farida Mgomi amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ileje.
Mhe. Mgomi amehaidi kuyafanyia kazi maazimio ya kikao hicho na kuendelea kusimamia shughuli zote za serikali ili kutimiza matarajio ya wananchi wa Ileje kupitia Serikali yao ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia kikao hicho Mhe. Mgomi amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na timu yake ya Wataalam, Wakuu wa Taasisi za Serikali ikiwemo TARURA, TANESCO, RUWASA, TFS NA TRA kwa ufafanuzi mzuri wa hoja zilizoibuliwa na Wajumbe na kuahidi kuendelea kutekeleza Ilani hiyo kwa vitendo.
Amesisitiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi mkubwa ili kuleta matokeo makubwa ya Serikali wilayani Ileje.