Home KITAIFA DC ILEJE AWAPONGEZA WALIMU KUSHINDA UMITASHUMTA

DC ILEJE AWAPONGEZA WALIMU KUSHINDA UMITASHUMTA

 

 

NA DENIS SINKONDE, SONGWE

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi ameshiriki hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi baada ya kufanikiwa kutwaa vikombe vinne kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa mwaka 2023.

Mhe. mgomi ameshiriki hafla hiyo Mei 31,2023 wakati akikabidhiwa vikombe vinne ambavyo wilaya ilishinda kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, na kugawa vyeti vya ushindi Kwa wanafuzi 12 waliochaguliwa kuuwakilisha mkoa kitaifa hafla iliyoandaliwa na idara ya elimu msingi wilayani hapa.

Mhe. Mgomi amesema lengo la kuandaa hafla hiyo ni kuwapongeza walimu na wanafunzi baada ya kufanikiwa kutwaa vikombe vinne kwenye mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa mwaka 2023 ambavyo ni Kikombe Cha mpira wa Netball, Usafi wa ndani wa wasichana, mziki wa kizazi kipya na Ngoma ya asili.

“Kutokana na kushinda vikombe hivyo nitagawa vyeti vya kutambua ushindi wenu kwa kuiheshimisha wilaya kimkoa hivyo tumieni vipaji vyenu Kwa manufaa yenu na wilaya bila kusahau kuendelea kujisomea muwapo shuleni”,amesema Mhe. Mgomi.

Mhe.Mgomi amewasihi wanafunzi na walimu kuhakikisha wanashinda vikombe vingi zaidi kama walivyoahidi kuleta vikombe vinne kwenye mashindano ya mwaka huu 2023.

Mhe.Mgomi amewataka walimu wa shule za msingi na sekondari kuendelea kushirikiana kuibua vipaji vya wachezaji Kwa lengo la kuandaa wachezaji watakaoleta ushindi kwenye wilaya yetu.

Mhe.Mgomi amewataka wanafunzi kuendelea kuwa na nidhamu pindi wanaposhiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzingatia taaluma ,Sanaa na michezo kwani vipo kwenye sera mbalimbali hapa nchini Ili kukitengeneza kizazi kinachopenda michezo.

Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo afisa mipango wilayani humo Amon Sangana amesema hafla ya kukutana na vijana hao ni sehemu ya kutia hamasa ya kuibua vipaji vya wanamichezo ,hivyo kuwasihi kuwa na nidhamu ili kuitumia nafasi hiyo kusonga mbele kimichezo.

“Niwapongeze walimu wanaosimamia michezo kuanzia shule za msingi na sekondari hivyo kama wilaya wataendelea kuibua vipaji vya wanafunzi kwani michezo ni ajira”, amesema Sangana.

Afisa elimu msingi wilayani humo Fikiri Mguye amesema Kwa mda mrefu wilaya hiyo haijawai kupata vikombe vya mashindano ya UMITASHUMTA Kwa shule za msingi hivyo Kwa mwaka huu tumefanikiwa kupata vikombe vinne

“Wilaya ya Ileje tumefanikiwa kutoa wanafunzi 12 watakaouwakilisha mkoa kwenye mashindano hayo kitaifa mkoani Tabora hivyo hamasa hiyo itasaidia Kwa mwaka 2024 tutatoa wanafunzi wengi kuuuwakilisha mkoa kitaifa”,amesema Mguye.

Katibu wa chama Chama mapinduzi wilayani hapo Hassani Lyamba amesema michezo ni sehemu ya kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama Cha mapinduzi ukurasa wa Ibara Ya 336 hadi 243 Zinazungumzia Utamaduni,Sanaa na Michezo na kuwaomba viongozi kuendelea kusimamia ibara hiyo ili kuibua vipaji vya vijana.

Akizungumza kwaniaba ya walimu Mpenzu amesema hamasa iliyotolewa ni chachu ambayo wanaahidi kuleta makombe mengi zaidi kwa wilaya kwenye mashindano watakayoshiriki.

Previous articleMWENYEKITI CHADEMA MKOA MBEYA AFUTIWA UANACHAMA
Next articleMTATURU AISHUKIA SERIKALI MRADI WA UMEME WA UPEPO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here