Home KITAIFA DC ILEJE AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA MAPOKEZI YA MWENGE

DC ILEJE AWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA MAPOKEZI YA MWENGE

Wananchi wilayani Ileje mkoani Songwe wameombwa kujitokeza kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Septemba 6, 2023 utakapowasili wilayani hapa kutokea Halmashauri ya Tunduma.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mheshimiwa Farida Mgomi ametoa wito huo kwenye kikao cha mwisho cha maamdalizi ya mapokezi ya mbio za mwenge wilayani hapa huku akiwasihi viongozi kuanzia ngazi ya vijiji na kata kuendelea na hamasa ya kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwenye mapokezi na kwenye mkesha utakaofanyika katika kijiji cha Ibaba kata ya Ibaba.

Mheshimiwa Mgomi amesema kila mwananchi analo jukumu la kupokea mwenge wa uhuru ambao utakimbizwa kwa kuzindua, kuweka mawe ya msingi kwenye baadji ya miradi ukiwepo mradi wa maji Ntembo kwenye tenki lililojengwa kijiji cha Mlale.

“Mwenge wa uhuru wilayani kwetu tutaupokea katika kijiji cha Mbebe kata ya Mbebe hivyo vikundi vya hamasa ,wananchi, utunzaji wa mazingira kama kauli mbiu inavyoelekezwa na kuonekana sisi tunashika nafasi ya kwanza kimkoa,” amesema Mhe. Mgomi

Mheshimiwa Mgomi amesema kila eneo mwenge wa uhuru utakapopita kwa ajili ya kukagua miradi ,na kuweka mawe ya msingi viongozi mhakikishe mnahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kwenye maeneo yote kwa lengo la kushangilia.

Hata hivyo wilaya ya Ileje itakabidhi mwenge wa uhuru katika wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya katika kijiji cha Ikuti na kuendelea na mbio hizo mkoani humo

Previous articleNMB YATOA MIL. 130/- KUDHAMINI BUNGE BONANZA
Next articleUBANGUAJI WA KOROSHO NCHINI CHANZO CHA ONGEZEKO LA FURSA ZA AJIRA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here