Home KITAIFA DC ILEJE AMBANA MHANDISI KUTOKAMILIKA KWA ZAHANATI

DC ILEJE AMBANA MHANDISI KUTOKAMILIKA KWA ZAHANATI

NA DENIS SINKONDE, SONGWE.

Mkuu wa wilaya ya Ileje, Farida Mgomi, ametoa siku tatu kwa mkuu wa idara ya ujenzi katika halmashauri hiyo Joramu Mayombo kujieleza kwanini mradi wa ujenzi wa zahanati ya Igoje kijiji cha Ilondo umesimama kwa zaidi zaidi ya mwaka mmja na nusu na kusabisha huduma za matibabu kutopatikana kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Mgomi amechukua hatua hiyo, baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia fundi aliyepewa kazi ya ujenzi wa zahaniti hiyo kutelekeza kazi na kufanya mradi kusimama kwa muda wote.

Baada ya malalamiko hayo, Mheshimiwa Mgomi alimwagiza mhandisi wa halmashauri kuwasiliana na fundi ili arejee na kuendelea na kazi.

“Suala sio kufika tuu eneo la mradi na kuendelea na ujenzi, lakini pia ndani ya siku tatu √†natokiwa anipatie taarifa juu ya nini kilikwamisha yeye (fundi) kutoendelea na kazi za mradi” alibainisha Mheshimiwa Mgomi.

Mheshimiwa Mgomi amesema mwaka 2021 serikali ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo ya Igoje iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi kwa kujenga boma kwa gharama ya shilingi milioni 19, lakini hadi kufikia sasa ujenzi haujakamilika kwa asilimia 100.

“Serikali imetoa fedha kusaidia nguvu ya wananchi, lakini cha kushangaza mhandisi unashindwa kusimamia na fundi anautekeleza mradi bila kuchukua htua yeyote kwa mujibu wa mkataba…haiwezekani fedha za serikali ziendelee kuchezewa” alisema Mgomi.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Enesta Kayuni amesema changamoto ya ukamilishaji wa zahanati hiyo ni usumbufu wa fundi aliyeingia mkataba kukamilisha sehemu ya zahanati ikiwepo uwekaji maji kwenye vyoo, vigae na gypsum

Mtendaji wa kijiji cha Ilondo Emmy Msukwa amesema, wajumbe wa kamati zilizoundwa kwenye ujenzi huo zinashindwa kumwajibisha fundi wakidai hawajaingia naye mkataba wakidai ofisi ya mkurugenzi imwajibishe.

Taarifa zilipatikana ni kwamba baadhi ya vifaa ikiwepo gypsum zimeanza kuharibika ,huku wakihofia ukamilishaji kutoisha kwani gharama za fundi ni shilingi milioni saba ambapo alilipwa zaidi ya shilingi milioni 5 na baki ni milioni moja na ushe ,hivyo mamlaka zinatakiwa kufuatilia juu ya matumizi ya fedha hizo.

Previous articleHAZINA SACCOS YATOA VITI MWENDO 15 BMH
Next articleNI VILIO NAULI MPYA ZA MABASI, DALADALA ABIRIA, MAKONDAKTA WASHIKANA MASHATI _ MAGAZETINI LEO DISEMBA 09/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here