Home KITAIFA DC ILEJE ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA ELIMU SHIRIKISHI YA USALAMA BARABARANI...

DC ILEJE ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA ELIMU SHIRIKISHI YA USALAMA BARABARANI KWA BODABODA

NA DENIS SINKONDE, SONGWE

MKUU wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Farida Mgomi amelitaka jeshi la polisi wilayani humo kutoa elimu shirikishi kwa waendeshaji wa vyombo vya moto pasipo kutumia mabavu.

Mgomi amesema hayo Julai 17,2023 katika ukumbi wa chama Cha Mapinduzi uliopo Itumba katika kikao cha pamoja na waendesha bodaboda na bajaji ambacho kiliandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM wilayani humo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mgomi amekemea vikali kamatakamata ya bodaboda bila kuwapa elimu ambayo itawasidia kuzijua sheria za usalama barabarani huku akiwataka ushirikiano wao kwa ulinzi na usalama wa wilaya yetu.

“Hakikisheni hawa vijana wanapokuja kwenye ofisi za serikali muwasikilizeni na kama changamoto zao zinaweza patiwa ufumbuzi kwa haraka wapeni bila kusahau kuwatembelea na kuwapa elimu kwenye vituo vyenu vya kazi”, amesema Mhe.Mgomi.

Mhe.Mgomi amewasihi madereva hao kufuata Sheria bila shuruti kwa kuzingatia maelekezo ya jeshi la polisi usalama barabarani bila kukimbia na kuwasihi wajenge ushirikiano na jeshi la polisi kuwasilisha changamoto zao.

Aidha Mhe. Mgomi amewasihi madereva hao kuwatumia viongozi wao kufika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ileje na Mkurugenzi halmashauri ya Ileje kuwaksilisha changamoyo zao wakae meza Moja na kuzitafutia ufumbuzi na kupeana uelewa wa pamoja.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo Hassan Lyamba amesema, chama hicho kimewakutanisha na viongozi wa serikali kwa lengo la kupeana uelewa wa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili na zile ambazo zitahitaji mda kuzipatia majibu zitataliwa kupitia wataalamu.

Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana CCM wilayani humo Diana Ngabo amesema kundi la vijana hao wamejiajiri Kwa lengo la kujiingizia kipato hivyo kukutana na viongozi hao kutawasidia kujuwa sehemu ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili.

“Jeshi la polisi tunawaomba msitumie mda mwingi kuwakamata bali wapeni elimu vijana hawa ambao ni madereva bajaji na bodaboda ili watambue sheria za usalama barabarani zitakazowasaidia kuepusha ajali zinazosababishwa na wao kukosa elimu,”amesema Ngabo.

Mmoja wa waendesha bodaboda aitwaye Blesi amesema, wakufunzi kutoka vyuo tofauti vya ufundi VETA maeneo tofauti yamekuwa yakitoa mafunzo kwa kushirikiana na jeshi la polisi wakiamini watapewa vyeti na leseni hali ambayo ilienda ndivyo sivyo.

Previous articleEWURA YATOA ONYO KWA KAMPUNI ZINAZOFICHA MAFUTA _ MAGAZETINI LEO JUMANNE JULAI 18/2023
Next articleSERIKALI YATOA MSAADA WA KIBINADAMU, NANYAMBA NA TANDAHIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here