Home KITAIFA DC ILEJE AKABIDHI PIKIPIKI KWA CHOMBO CHA KUSIMAMIA MAJI KATA YA BUPIGU(CBWSO).

DC ILEJE AKABIDHI PIKIPIKI KWA CHOMBO CHA KUSIMAMIA MAJI KATA YA BUPIGU(CBWSO).

 

NA DENIS SINKONDE, SONGWE

Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe. Farida Mgomi amekabidhi pikipiki aina ya TVS kwenye chombo cha usimamizi huduma ya maji ngazi ya jamii Cha muungano(CBWSO) kata ya Bupigu wilayani humo Ili kurahisisha kutoa huduma.

Akikabidhi pikipiki hiyo Mhe. Mgomi amesema lengo la kukubidhi pikipiki hiyo ni kumrahisishia fundi kufika Kwenye eneo lenye changamoto ya maji kwa haraka na kuitatua.

Mhe. Mgomi amesema pikipiki hiyo imekabidhiwa Kwa ajili ya fundi ambaye jukukumu lake ni kutembelea maeneo yatakayoripotiwa kuwa na changamoto hususani kwenye jumuiya hiyo inayounganisha vijiji vya Chabu na Bupigu katika kata ya Bupigu wilayni humo.

“Nimarufuku kutumia pikipiki hiyo kama bodaboda ,au kubebea magendo ukibainika tutakushughulikia kwani RUWASA wilaya Ileje imenunua kwa lengo la kuhakikisha unafika kwa wakati eneo lenye changamoto ya kutotoa maji”,amesema Mhe.Mgomi.

Mhe. Mgomi amewasihi wanajumuiya hao kuitunza pikipiki hiyo Ili Idumu kwa muda mrefu, na kuhakikisha RUWASA inafurahia jumuiya kutoa huduma tarajiwa kwenye jamii na kuwa mfano kwa jumuiya zingine wilayani hapa.

Mwenyekiti wa chombo hicho Bahati Mlungu amesema chombo hicho kilianzishwa mwaka 2023 kisheria na mpaka sasa kina jumla ya watumiaji maji 3346 hivyo pikipiki hiyo itakuwa msaada kutatua changamoto zinazojitokeza.

Fundi aliyeajiriwa na chombo hicho Emmanuel Musa Simwika amemwahidi mkuu wa wilaya kuitumia pikipiki hiyo kwa lengo lililohitajika hivyo kuwaaihi wanajumuiya na wananchi kutoa taarifa ya changamoto pindi inapotokea kwenye vijiji hivyo ili afike kwa wakati kutatua.

Previous articleJUMUIYA ZA WATUA MAJI ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIRADI KWA WELEDI
Next articleJUMUIYA ZA WATUMIA MAJI ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIRADI KWA WELEDI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here