Home KITAIFA DC ILEJE AHITIMISHA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA MKOA SONGWE

DC ILEJE AHITIMISHA MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA MKOA SONGWE

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkaoni Songwe Mhe. Farida Mgomi amewataka wanamichezo kuvilinda na kuheshimu vipaji vyao Ili kujitengenezea uchumi na kuondokana na utegemezi kupitia michezo.

Akizungumza na wanachezo ambao ni wanafunzi wakati akifunga mashindano ya UMISSETA ngazi ya mkoa Juni 5,2023 katika viwanja vya shule ya sekondari Ileje ambako mashindano yamefanyika kimkoa wilayani Ileje Mhe. Mgomi amesema wanatarajia mkoa huo unarudi na kombe la kitaifa kwani timu iliyochaguliwa itauwakilisha vyema mkoa.

Mhe. Mgomi amewataka wanafunzi hao kucheza kwa bidii na nidhamu ili kupata wachezaji bora kisha timu bora ya Mkoa wa Songwe itakayopelekea (kunyakua) kushinda makombe yote huko Tabora ambapo mashindano haya yatafanyika kitaifa.

“Niwakumbushe kwamba michezo inaweza kukuinua kiuchumi kwani kwa ulimwengu wa sasa imekuwa ni ajira, hivyo msibeze vipaji vyenu bali viheshimuni na kuviendeleza”, amesema Mgomi.

Katika hatua nyingine Mhe.Mgomi amekabidhi vikombe kwa timu wilaya zilizofanya vyema kwenye mashindano hayo ngazi ya mkoa ambapo wilaya ya Mbozi imekuwa mshindi wa kwanza Kwa mashindano kiujumla.

Hata hivyo Mhe.Mgomi ametumia nafasi hiyo kupongeza ushiriki mkubwa wa wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Songwe.

“Jumla ya wanafunzi 600 walishiriki mashindano hayo kutoka halmashauri tano za mkoa wa Songwe ambapo wamechagua wachezaji 120 wa michezo tofauti tofauti kuuwakilisha mkoa kitaifa mkoani Tabora”, amesema Mhe. Mgomi.

Aidha Mhe. Mgomi amesema kuwa michezo hii hufanyika kila mwaka na kwa mwaka huu michezo inayochezwa na wanafunzi hao ni pamoja na mpira wa miguu, riadha, volleyball, basketball na netball.

Previous articleMKEKA WA UTEUZI NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA NA WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI ZA SERIKALI ZA MITAA HUU HAPA
Next articleAJALI YA FUSO NA NOAH YAJERUHI 8 MIKUMI MOROGORO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here