Home KITAIFA DC BULEMBO: SITAFUMBIA MACHO MGOGORO WOWOTE WA ARDHI UNAOSABABISHWA NA VIONGOZI AU...

DC BULEMBO: SITAFUMBIA MACHO MGOGORO WOWOTE WA ARDHI UNAOSABABISHWA NA VIONGOZI AU WANANCHI

 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo amewataka wamiliki wa ardhi walionunua ardhi katika maeneo ya kigamboni wahakikishe wanayaendeleza vinginevyo watanyang’anywa maeneo hayo na kugawia wananchi

Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake ya mtaa kwa mtaa ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majawabu aliyoifanya katika Mtaa wa Kichangani ,Nyange na Tundwi Songani iliyopo kata ya Pemba Mnazi.

Mkuu wa wilaya Bulembo alisema kuwa kuna maeneo mengi ni mapori hayaendelezwi ” mtu akivamia tunatengeneza migogoro” alisema nakuongeza kuwa mmiliki yoyote wa ardhi ambaye hata endeleza kama wilaya watachukua hatua kwa kuishauri Mamlaka husika kufuta hati ili maeneo hayo wayagawe kwa wananchi wengine wenye uhitaji wa ardhi.

“Kigamboni nzima kuna migogoro mingi ya ardhi na migogoro mingine inasababishwa na wananchi wenyewe na mingine inasababishwa na viongozi wetu” Alisema Bulembo nakuongeza kuwa hatafumbia macho mgogoro wowote unaosababishwa na wananchi au viongozi .

Mkuu wa Wilaya huyo alisisitiza kuwa Sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka1999 inaelekeza kuwa mtu yeyote atakayeshindwa kuendeleza eneo lake kwa miaka mitatu atanyanganywa ardhi kwa mujibu wa Sheria na taratibu.

Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Kigamboni Daimon Mpoki amekiri kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi katika manispaa ya kigamboni ambapo amesema wamekuwa wakiishughulikia kwa kutoa elimu mbalimbali ya masuala ya ardhi kwa wananchi.

Bulembo ameanza rasmi ziara ya mtaa kwa mtaa yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi ambapo. Wilaya hiyo ya kigamboni ina Tarafa 3,kata 9 na Mitaa 67

 

Previous articleJUMUIYA ZA WATUMIA MAJI ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIRADI KWA WELEDI
Next articleVIGOGO SABA NHIF KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI _ MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JUNI 03/2023

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here